
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), linakemea tabia inayokithiri ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii inayolihusisha Jeshi na Siasa kwa lengo la kupotosha Umma na kuzua taharuki.
Katika Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Bernard Mlunga, Novemba 12,2025 limeutaka Umma kupuuza tangazo linaloonekana likisambaa mtandaoni lenye maudhui ya maandamano kuwa ni uzushi wenye lengo la kuadaa wananchi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa Amani Nchini, hivyo lipuuzwe.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, JWTZ linaendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaojihusisha na upotoshaji huo.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!