Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia: Nafasi ya Waziri Mkuu si ya ndugu wala rafiki, ni ya Watanzania – Video

  • 13
Scroll Down To Discover

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kutumia nafasi aliyopewa kuwatumikia Watanzania wote bila upendeleo wa aina yoyote.

Akizungumza leo Novemba 14, 2025 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kumuapisha Dkt. Mwigulu, Rais Samia alisema nafasi hiyo ni ya kitaifa na siyo ya marafiki, ndugu au jamaa.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

“Mzigo huu si mdogo kwa umri wako, mzigo huu ni mkubwa. Kwa umri wako vishawishi ni vingi vya marafiki, ndugu na jamaa. Nafasi yako ile haina ndugu, haina rafiki, haina jamaa; ni nafasi ya kulitumikia taifa hili,” alisema Rais Samia.

Aidha, alimtaka Waziri Mkuu mpya kuhakikisha anaweka mbele maslahi ya wananchi na kusimamia kwa uadilifu majukumu yote aliyokabidhiwa.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba miongozo ya utendaji kazi mara baada ya kumuapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.



Prev Post Vibonge Kunyimwa Visa? Haya Ndiyo Mapya Kutoka Serikali ya Rais Trump
Next Post Dkt. GeorDavie Atemuliwa Balozi wa Afrika Mashariki na UN-PAF
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook