

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameahidi kusimamia kwa nguvu zote utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, akisema anaufahamu vyema umasikini kwani ameishi kwenye hali hiyo kwa muda mrefu.
Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma, wakati akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuthibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Amesema serikali itahakikisha mipango yote ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia hali halisi ya wananchi, hususan wale wa kipato cha chini.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!