Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Amshukuru Dkt. Mpango kwa Mchango Mkubwa Katika Awamu ya Sita

  • 19
Scroll Down To Discover

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza na kumshukuru Makamu wa Rais Mstaafu  Dkt. Philip Mpango kwa mchango aliyoutoa wakati wa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita, ambayo ilitoa urahisi wakati wa ufanyaji kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Makamu wa Rais amesema ataendeleza jukumu la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezo wake wote ili kutekeleza vema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaletea wananchi maendeleo.

Pia amemsihi, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango kuendelea kutoa mchango wake pale utakapohitajika, katika utekelezaji wa sera mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwemo masuala ya uchumi wa buluu.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa nafasi hiyo muhimu na kumsihi kutekeleza vema majukumu ya kuwa mshauri namba moja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemsihi kutumia hekima na unyenyekevu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa nyaraka mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais, kutoka kwa mtangulizi wake, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.
Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiombewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MDkt. Philip Mpango, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

 



Prev Post Rais Dkt.Samia amteua Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Next Post CCM Yatoa Fomu za Uteuzi wa Spika na Naibu Spika wa Bunge 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook