Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Jumanne 22 April 2025

  • 21
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Jumanne 22 April 2025

Rais wa heshima na mwekezaji wa Simba SC Mohamed Dewji ametumia ukurasa wake wa Instagram kumkingia kifua kiungo mshambuliaji Jean Cherles Ahoua kufuatia kukosa bao la wazi
katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrka Kusini jana Jumapili visiwani Zanzibar.

Mo Dewji ameandika: Wanasimba,

Jean-Charles Ahoua ni mmoja wa wachezaji waliotupa sababu nyingi za kushangilia msimu huu, licha ya vyote amekuwa sehemu ya mafanikio yetu.

Kwa kosa moja lilitokea tunaweza kumsema vibaya leo, ila tukumbuke: hata mastaa wa dunia kama Fernando Torres waliwahi kukosa magoli ya wazi — kwenye mechi kubwa kama Chelsea dhidi ya Manchester United. Hii ni soka. Haya ni mambo ya kawaida kwenye mchezo huu.

Lakini jambo kubwa zaidi ni namna tunavyochagua kusimama baada ya kila tukio. Tunajifunza, tunaimarika, na tunaendelea kupambana.

Mchezo wetu dhidi ya Stellenbosch bado uko mbele. Safari haijaisha. Na huu si wakati wa kulaumiana — ni wakati wa kuungana na kua kitu Kimora.

Simba inajengwa juu ya mshikamano. Tunasimama na Jean-Charles. Tunasimama na kila mchezaji anayejitoa kwa jezi hii. Na tunaendelea na vita iliyokua mbele yetu.

Simba ni familia. Simba ni nguvu moja.



Prev Post Rais Samia Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Baba Mtakatifu Francisko
Next Post Bodaboda, Wamachinga, na Walemavu Wagomea Maandamano ya Aprili 24
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook