
Rais Samia Suluhu Hassan, ameungana na viongozi wengine duniani kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Rais Samia ameandika:
“Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko.
“Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani.
“Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina.”
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!