

Umoja wa Maafisa Usafishaji maarufu kama waendesha Bodaboda na Bajaj, Umoja wa Wamachinga na Wenye Uhitaji maalum (Walemavu) wote kwa pamoja leo wametangaza kuyagomea maandamano yaliyohamasishwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ siku ya Aprili 24 mwaka huu.

Wote kwa pamoja wameyagomea maandamano hayo ya kukusanyika Mahakama ya Kisutu jijini Dar ambapo kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu itakuwa mahakamani hapo.

Wote kwa pamoja walidai wamechoka kutumiwa vibaya na wanasiasa ambao mwisho wa siku wakipatwa na matatizo wanatelekezwa.

Kwa upande wao Bodaboda wamekumbushia mmoja wa viongozi wa CHADEMA alivyowahi kuwaambia kuwa kazi yao ni ya laana. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!