
Mtoto wa kiume, Samiu Salim, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, amefariki dunia baada ya kuzama kwenye maji ya Mto Faeli katika mtaa wa Mruki, mjini Babati, mkoa wa Manyara. Tukio hilo limetokea Aprili 19, 2025, majira ya saa 9 alasiri.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa na baba yake ambaye alikuwa akifanya shughuli zake kandokando ya mto huo. Hata hivyo, baada ya kumaliza shughuli zake, baba huyo hakumuona tena mtoto wake na alikuta viatu vya plastiki (yebo yebo) katika eneo alilomuacha. Hapo ndipo alipotambua kuwa mtoto alikuwa tayari amezama mtoni.
Baada ya juhudi za uokoaji, mwili wa mtoto ulipatikana umbali kidogo kutoka alipozamia, akiwa tayari amefariki dunia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!