
Muwekezaji kutoka Ulaya, Siriviea Vrascam, amefichua hali ya kusikitisha aliyoipitia baada ya kudai kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na mwanaume aliyejitambulisha kama askari wa usalama, ambaye alimtupa kwa nguvu nje ya shamba lake la maua lililopo mkoani Kilimanjaro.
Bi. Vrascam amesema kuwa tukio hilo lilitokea ghafla, bila nyaraka wala agizo lolote la kisheria. Anaeleza kuwa alitoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi na kufungua kesi rasmi yenye kumbukumbu namba RB No: MOS/RB/8476/024.
Kwa kushirikiana na vyombo vya habari, Global TV ilifanya jitihada za kufuatilia maendeleo ya shauri hilo kwa kuwasiliana na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro. Simu ilipokelewa na Kaimu Kamanda, ambaye alikiri kutokuwa na taarifa kuhusu tukio hilo, lakini aliomba namba ya RB kwa ajili ya kufuatilia jarada la kesi hiyo kwa undani zaidi.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi kuhusu hatua zilizochukuliwa—hali inayoibua maswali kuhusu ufanisi wa ulinzi kwa wawekezaji wa kigeni.
Bi. Vrascam ametoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan, akimuomba kuangalia upya mfumo wa ulinzi na usimamizi wa haki za wawekezaji, hasa wanawake, wanaokumbana na changamoto kama hizo.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!