Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kikwete Awakilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Waziri Mkuu wa Congo

  • 8
Scroll Down To Discover

Rais wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), COLLINET MAKOSSO Anatole.

Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.

Tukio hilo lilifanyika jijini Brazzaville Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.

Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.



Prev Post Dkt. Philip Mpango: Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji
Next Post Chadema: INEC Haina Mamlaka ya Kuiondoa Kwenye Uchaguzi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook