Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina Ajificha Baada ya Jaribio la Kumuua

  • 6
Scroll Down To Discover

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema amejificha mahali salama kufuatia jaribio la kumuua lililoripotiwa kutokea baada ya wiki kadhaa za maandamano makubwa yanayomtaka ajiuzulu.

Katika hotuba ya moja kwa moja kwa taifa kupitia ukurasa wake wa Facebook, Rajoelina, mwenye umri wa miaka 51, alisema kuwa kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua, na kuongeza kuwa amelazimika kujihifadhi ili kulinda maisha yake.

Rais huyo hakueleza aliko kwa sasa, ingawa ripoti ambazo bado hazijathibitishwa rasmi zimependekeza kuwa huenda alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

Nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari ya Hindi imekuwa ikikumbwa na maandamano makubwa yanayoongozwa hasa na vijana wanaojiita “Gen Z Mada”, wanaomtaka Rais Rajoelina aondoke madarakani. Waandamanaji hao wamekuwa wakilalamikia hali ngumu ya maisha, ukosefu wa ajira, na kile wanachokiita utawala wa kiimla.

Jaribio la Rajoelina kuwatuliza waandamanaji hao lilishindikana licha ya kufuta baraza lake lote la mawaziri na kuunda serikali mpya, hatua iliyolenga kupunguza shinikizo la kisiasa.

Rajoelina hajaonekana hadharani tangu Jumatano iliyopita, huku ofisi yake ikithibitisha mwishoni mwa wiki kuwa kulikuwa na jaribio la kumlazimisha kuondoka madarakani.

Hotuba yake kwa taifa, iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumatatu, ilicheleweshwa mara kadhaa kutokana na hali ya machafuko jijini Antananarivo, ambapo wanajeshi waliripotiwa kutishia kuteka makao makuu ya televisheni ya taifa.

Hatimaye, katika hotuba yake iliyotangazwa kupitia Facebook, Rajoelina alisema:

“Tangu Septemba 25 kumekuwa na majaribio ya kuniua na ya kufanya mapinduzi. Kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua. Nililazimika kutafuta mahali salama ili kulinda maisha yangu.”

Akaongeza:

“Kuna njia moja tu ya kutatua masuala haya; ni kuheshimu katiba na misingi ya demokrasia.”

NDANI ya MSIKITI ALIOJENGA FARID MUSSA wa YANGA – AUPA JINA la MAMA YAKE – ”AISHA”…



Prev Post Waziri Mkuu Majaliwa, Makamu Wa Rais Dkt. Mpango Wahudhuria Ibada Ya Kumuombea Mwalimu Nyerere Mbeya
Next Post Farid Musa Asifiwa kwa Utu na Unyenyekevu Nje Soka, Ajenga Msikiti – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook