
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameshiriki leo, Oktoba 14, 2025, katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa, Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, pia alihudhuria ibada hiyo, ikionesha mshikamano wa viongozi wa nchi katika kumbukumbu za Baba wa Taifa.
Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Mhashamu Gervas Nyaisonga, huku wakiombea amani, mshikamano wa taifa, na baraka kwa wananchi wa Tanzania.
Tukio hilo limekuwa fursa kwa viongozi na wananchi kuenzi urithi wa uongozi wa Hayati Mwalimu Nyerere, akisisitiza maadili ya mshikamano, utu, na maendeleo ya taifa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!