Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia: Uchaguzi si Vita, Ni Tendo la Demokrasia Tukapige kura, Turudi Nyumbani – Video

  • 56
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza Septemba 17, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi – Zanzibar, Dkt. Samia amesisitiza kuwa uchaguzi ni zoezi la kidemokrasia, hivyo wananchi wanapaswa kupiga kura kwa utulivu na kurejea nyumbani bila vurugu.

“Uchaguzi si vita, ni tendo la demokrasia. Niwaombe ndugu zangu, twende tukapige kura kwa utaratibu, turudi nyumbani ili nchi ibaki salama,” alisema Dkt. Samia huku akionya kwamba kushika silaha, iwe ya kijadi au ya kisasa, hakutaleta suluhu ya maana kwa taifa.

Dkt. Samia alihitimisha kwa kusisitiza kuwa amani ya Tanzania ni nguzo kuu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania hasa kipindi hiki cha uchaguzi.



Prev Post Kesi ya Uhaini Dhidi ya Tundu Lissu Kuendelea Leo Mahakama Kuu, Dar
Next Post Rais Chekera wa Malawi Anaelekea Kushindwa Uchaguzi Mkuu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook