Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Viongozi wa CHADEMA Wakabiliwa na Kesi ya Jinai, Waitwa Mahakamani Jumatano

  • 7
Scroll Down To Discover

Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara, John Heche.

Kesi ya jinai namba 25480 ya mwaka 2025, inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara, John Heche, imepangwa kusikilizwa kesho, Jumatano Oktoba 15, 2025, mbele ya Jaji Awamu Mbagwa.

Kesi hiyo imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, pamoja na wenzake wawili, Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu.

Taarifa ya wito iliyotumwa kwa Wakili wa viongozi hao, Dkt. Rugemeleza Nshala, kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imeeleza kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa majira ya saa 03 asubuhi.

Mbali na John Heche, washtakiwa wengine ni:

John Mnyika – Katibu Mkuu

Rose Mayemba – Mjumbe wa Kamati Kuu

Brenda Rupia – Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Hilda Newton – Mjumbe wa Baraza Kuu

Twaha Mwaipaya – Mwenezi wa zamani BAVICHA Taifa

Gervas Benard Lyenda – Afisa kutoka Kurugenzi ya Habari na Uenezi

Pia, baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA wamejumuishwa kwenye kesi hiyo kutokana na nafasi zao katika chama.

Washtakiwa wanadaiwa kukiuka amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, iliyotolewa Juni 10, 2025, iliyopiga marufuku wadaiwa kujihusisha na shughuli zozote za kisiasa na matumizi ya rasilimali za chama hadi kesi ya msingi itakapotolewa maamuzi. Kesi ya msingi inahusu mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na inaendelea kusikilizwa chini ya Jaji Hamidu Mwanga.

Kesi hii imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari na wadau wa siasa kutokana na umuhimu wake katika taswira ya kisiasa na utaratibu wa kisheria nchini.

WAKILI wa TUNDU LISSU AZUNGUMZA kwa UCHUNGU POLISI KUWAKAMATA KILA SIKU WAFUASI wa CHADEMA



Prev Post Farid Musa Asifiwa kwa Utu na Unyenyekevu Nje Soka, Ajenga Msikiti – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook