Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kikwete atembelea makazi ya Mfalme Haile Selassie mjini Addis Ababa

  • 13
Scroll Down To Discover

ADDIS ABABA-Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametembea Qasir la Taifa la Ethiopia ambalo lilikuwa makazi ya Mfalme Haile Selassie.

Kikwete alitembelea Qasir hilo kufuatia maombi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dkt. Abiy Ahmed ambapo walikutana jijini Addis Ababa Aprili 11, 2025 kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Qasir hilo ambalo kwa sasa limegeuzwa kuwa makumbusho ni eneo muhimu kwa kuwa limekusanya urithi wa utamaduni wa Ethiopia ambao kimsingi bado haujatumika ipasavyo kwa faida ya wananchi wa Taifa hilo.
Awali, Kikwete alikutana na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wakiongozwa na Balozi Innocent Shiyo na kuwasihi kushikamana na utamaduni wa Tanzania ambao miaka yote umekuwa ukihamasisha umoja barani Afrika.



Prev Post Wakandarasi 457 Wa Ujenzi Wa Barabara Walipwa, Wengine 322 Kulipwa
Next Post Dkt. Kikwete Aupokea Mwenge wa Uhuru Msoga, Chalinze
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook