Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Nelly Kamwelu Amuangukia Mama Yake

  • 11
Scroll Down To Discover

Muigizaji na Mwanamitindo, Nelly Kamwelu amemuomba msamaha mama yake na kukiri kuwa mapenzi yalimtawala akili kufikia hatua ya kutosikiliza ushauri wake mpaka kufikwa na majanga ya kupewa kipigo na aliyekuwa mpenzi wake

Akizungumza kupitia Mashamsham ya Wasafi FM, Nelly Kamwelu amesema kuwa kwa sasa anasikiliza nini mama yake anamuambia kwani madhara ya kutosikiliza ameyashuhudia kwa macho yake

Wiki kadhaa zilizopita, muigizaji huyo alijikuta akiuguza majeraha mwili mzima baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi

Mbali na hayo, pia Nelly Kamwelu ameeleza namna familia ya aliyekuwa mpenzi wake ilivyomtorosha kijana wao kwa kumsafirisha ingalikuwa bado kuna kesi polisi

Nelly amesema amesamehe yote aliyofanyiwa na mwanaume huyo ila ameweka wazi kuwa hawezi kurudiana naye kamwe

The post Nelly Kamwelu Amuangukia Mama Yake appeared first on Wasafi Media.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Ijumaa 11 April 2025
Next Post Msajili wa Vyama: Kauli ya “No Reform, No Election” Haijavunja Sheria, Uchaguzi 2025 Uko Pale Pale
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook