Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump atishia kuiongezea China ushuru mwingine wa asilimia 50

  • 8
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuiwekea China ushuru wa ziada wa asilimia 50 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani ikiwa haitafuta ushuru wake wa kulipiza kisasi wa asilimia 34.

China ilijibu vikali Jumapili baada ya Trump kutangaza ushuru huo mpya kwa bidhaa zake. Hata hivyo, Trump ameipa Beijing muda wa saa 24 kufuta ushuru wake, la sivyo bidhaa za China zitakabiliwa na ongezeko hilo la ushuru.

Katika hatua yake ya kujibu, China imesisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa na kwamba itapambana hadi mwisho dhidi ya nyongeza mpya ya ushuru kutoka Marekani.

Ushuru huo mpya unaweza kuacha baadhi ya makampuni ya Marekani yanayoleta bidhaa fulani kutoka China yakikabiliwa na ushuru wa asilimia 104.

The post Trump atishia kuiongezea China ushuru mwingine wa asilimia 50 appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Waziri wa Mawasiliano Afrika Kusini ashutumiwa kwa kujaribu kubadilisha sheria ya umiliki kwa kampuni ya Elon Musk
Next Post Rais Samia Atembelea Makumbusho Ya Hayati Neto Nchini Angola
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook