Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Waanza Uchunguzi wa Tuhuma za Utekwaji wa Humphrey Polepole

  • 65
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na Augustino Polepole kuhusu madai ya kutekwa kwa ndugu yake, Humphrey Polepole.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi leo Oktoba 7, 2025, jalada la uchunguzi lilifunguliwa mara baada ya taarifa hizo kusambaa jana, Oktoba 6, 2025.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mbali na kukusanya maelezo kutoka kwa watu mbalimbali, Polisi wanaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili atoe ushirikiano na maelezo ya kina kuhusu madai hayo, ikiwemo uthibitisho wa madai yake kwamba Afisa wa Polisi alihusika katika tukio hilo.

Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi pia unalenga kubaini kama kweli Humphrey Polepole alikuwa mkazi au mpangaji wa nyumba ambako inadaiwa tukio hilo lilifanyika.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, jijini Dodoma.



Prev Post Mariam Mwinyi Awasisitiza Wanawake Pemba: “Tumuunge Mkono Dkt. Mwinyi…”
Next Post Kwa nini bado vita vya Israel huko Gaza vinaendelea baada ya miaka miwli? Katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook