Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JWTZ Latoa Ufafanuzi Rasmi Kuhusu Upotoshaji Mitandaoni – Video

  • 94
Scroll Down To Discover

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko kali kufuatia kuenea kwa taarifa na mijadala mitandaoni inayolihusisha jeshi hilo na masuala ya kisiasa, likionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa leo jijini Dodoma na msemaji wa JWTZ, Kanali Gaudentius Ilonda, jeshi limesema limeanza kufuatilia kwa karibu watu na kurasa za mitandao ya kijamii zinazojihusisha na kusambaza taarifa zenye lengo la kulichafua au kulipotosha jeshi hilo mbele ya umma.


“JWTZ halijihusishi na siasa. Wajibu wetu ni kulinda mipaka, uhuru na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeona mitandao kadhaa ikijaribu kulitumia jina la jeshi vibaya, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi,” amesema Kanali Ilonda.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Dansa Maarufu wa Tukuyu Sound, Arafa Matatuu, Afiwa na Mume
Next Post Dkt. Nchimbi Aendelea na Kampeni Tabora, Awaomba Wananchi Kumpigia Kura Dkt. Samia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook