Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TANESCO Yatoa Tahadhari Kwa Wateja Kuhusu Changamoto ya Malipo ya Umeme

  • 10
Scroll Down To Discover

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kuwa kumetokea changamoto ya manunuzi ya umeme (LUKU) hali inayosababisha Wateja wake kushindwa kununua umeme kupitia njia za mitandao ya simu, Mawakala pamoja na njia za kibenki.

Katika taarifa yake kwa Umma, TANESCO imesema kupitia Wataalamu wake imejiridhisha kuwa changamoto hii inasababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa malipo ya Serikali (GePG) ambapo tayari Wataalamu wa mfumo huo wanashughulikia changamoto iliyojitokeza ili huduma iweze kurejea katika hali ya kawaida.

“TANESCO inatoa wito kwa Wataalamu wa GePG kushughulikia jambo hili kwa umuhimu mkubwa ili kuwaondolea Wateja usumbufu wa kushindwa kufanya manunuzi ya umeme kunakosababishwa na changamoto hiyo, Shirika litawafahamisha Wateja wake huduma zitakaporejea kikamilifu”



Prev Post ALAF Yazindua Mpango wa Siku Mbili wa Elimu ya Afya kwa Wafanyakazi
Next Post Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa UDART
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook