Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mtoto wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Abbas Ali Mwinyi, Afariki

  • 1
Scroll Down To Discover

Mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Ndugu Abbas Ali Mwinyi, ambaye pia ni kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefariki dunia leo akiwa Hospitali ya Lumumba, mjini Unguja leo, Septemba 25.

Marehemu Abbas Ali Mwinyi alijulikana kwa nafasi yake kama msemaji wa familia mara baada ya kifo cha Baba yao, ambapo alisimama mbele ya vyombo vya habari na kueleza msimamo pamoja na taarifa muhimu za kifamilia.

Aidha, kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa mgombea rasmi wa Ubunge wa Jimbo la Fuoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuchaguliwa kuwania tena nafasi hiyo.



Prev Post Jenerali Mkunda Ampongeza Sajinitaji Simbu 
Next Post Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Na Kuokoa Ndoa Yako Kutoka Kwa Mitego Ya Mpango Wa Kando
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook