Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

RECAP: Kenya wanawekeza katika Muziki bora kuliko Bongo – El Mando

  • 8
Scroll Down To Discover

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz anasema Muziki wa Kenya umeanza kuamka tena baada ya kusua sua kwa miaka kadhaa.

Ukiangalia mwenye upande wa Wasanii wa kuimba ubora wao umeongezeka sana ukiwatolea mfano watu kama Sauti Sol akiwemo Bien lakini pia Bensoul na wengine.

Ukija mwenye upande wa Hip Hop Khaligraph Jones anazidi kupambana kwa nafasi yake na Hip Hop ya Kenya ipo kwenye mikono salama.

Kwa Tanzania ukiwatoa Diamond na Alikiba ambao wao kwa sasa hawafanyi tena muziki wa Ushindani zaidi maana wameshafanikiwa hawana kitu cha Ku-Prove hatuna wasanii wengine level zao.

Hii inatoa ishara mbaya sana kwa game ya Bongo Fleva maana wasanii wa Kenya wamejua wapi Watamzania wanakosea au Udhaifu wao upo wapi.

Anaongeza kuwa Taifa la Kenya litakuwa taifa la Kwanza kwa msanii wao kushinda GRAMMY tofauti na Tanzania maana wasanii wa Tanzania hawajawekeza kwenye Quality ya muziki.

Ametolea mfano BIEN ana Tour yake Marekani na Ulaya.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman & Editor @samirkakaa



Prev Post RECAP: Bongo Fleva imeshuka Wasanii wanawekeza kwenye branding sio quality – El Mando
Next Post RECAP: Kenya watashinda Grammy kabla ya Bongo – El Mando
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook