

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), Annalena Baerbock ameuambia mkutano wa suluhisho la mataifa mawili uliofanyika makao makuu ya umoja huo jana Jumatatu: kuwa “nchi-dola huru ya Palestina lazima ianzishweâ€.
Baerbock akaongeza: “hali halisi ya watoto wa Ghaza ni vita na uharibifu. Wengi wameuawa huko Ghaza bila ulimwengu kujua majina yao.â€
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amefafanua katika hotuba yake hiyo kwa kusema: “ulimwengu umewaangusha watoto wa Ghaza. Watoto wote katika Mashariki ya Kati wanastahili kuishiâ€.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Baebock amesema: “tunahitaji usitishaji vita wa haraka na bila masharti huko Ghaza. Hamas lazima iwaachilie mateka wote mara moja na bila mashartiâ€.
Rais huyo ni Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani amewaeleza washiriki wa mkutano wa suluhisho la nchi-dola mbili: “hali ya kutisha ya Gaza inaonyesha kwamba hatuwezi kuruhusu uharibifu kama huo utokee tena. Hali ya Ghaza haikubaliki na vita lazima vikomeâ€.
Baerbock amesisitiza kwa kusema: “nchi huru na endelevu ya Palestina lazima ianzishwe. Hamas inapaswa kuweka chini silaha zake na kuhitimisha utawala wake huko Ghazaâ€. Rais wa sasa wa Palestine ni Mahmoud Abbas











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!