Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Nchimbi Atikisa Ludewa, Aeleza Dkt. Samia Atakavyotekeleza Ilani ya CCM Baada ya Uchaguzi

  • 2
Scroll Down To Discover


MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Ludewa mkoani Njombe, Jumatatu Septemba 22,2025 kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea Mkoa wa Ruvuma.Dkt.Nchimbi amewasili kwenye uwanja wa mpira wa Ludewa na kupokewa na Viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwasalimia Wananchi kabla ya kuwahutubia.






Akiwa katika mkutano huo,Dkt Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine atawahutubia Wananchi wa jimbo la Ludewa na kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa,Ndugu Joseph Zacharius Kamonga na Madiwani.
Dkt. Nchimbi anaendelea kuinadi Sera na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inakwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.Aidha,amekuwa akitumia nafasi hiyo pia kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025



Prev Post Kim Jong Un: Tuko Tayari Kuzungumza na Marekani Ila Tusiondolewe Silaha za Nyuklia
Next Post Nilichoka Na Kejeli Za Watu Kuhusu Ndoa Yangu, Hatua Niliyopiga Ilibadilisha Maisha Yetu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook