
Katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa mchango chanya kwa jamii, leo kampuni ya Meridianbet imefanya zoezi maalum la ugawaji wa vifaa vya kujilinda wakati wa shughuli za usafi kwa wasafishaji wa barabara katika Manispaa ya Kinondoni.
Zoezi hilo lililofanyika katika ofisi za Manispaa ya Kinondoni limehusisha ugawaji wa vifaa mbalimbali muhimu kama vile glovu, barakoa, buti za kazi, pamoja na reflector jacket kwa wasafishaji wa barabara wanaofanya kazi kwa bidii kuhakikisha mji unakuwa safi na salama kwa wakazi wake.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi kutoka Meridianbet alisema:
“Hawa ni mashujaa wa afya ya jamii yetu. Kazi yao ni ngumu lakini ya muhimu sana. Kama Meridianbet, tunatambua mchango wao mkubwa na tumeona ni vyema kuonyesha kuthamini kazi yao kwa kuwapatia vifaa vya msingi vya kujikinga na mazingira hatarishi wanapokuwa kazini.”
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Manispaa ya Kinondoni aliishukuru Meridianbet kwa msaada huo na kueleza kuwa ni mfano bora wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali katika kuinua ustawi wa wafanyakazi wa ngazi ya chini.
“Hili ni jambo la faraja na matumaini. Tunapenda kuona kampuni kama Meridianbet zinaonyesha moyo wa huruma na kushirikiana nasi katika kulinda afya na usalama wa watumishi wetu.”
Zoezi hili ni sehemu ya mpango mpana wa Meridianbet wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), ambapo kampuni imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi mbalimbali ya jamii kwa kutoa misaada ya kijamii, elimu, afya, na ustawi wa vijana kupitia michezo.
Kwa kuendeleza shughuli kama hizi, Meridianbet inaendelea kuthibitisha kuwa si tu kinara katika burudani ya michezo ya kubahatisha, bali pia mshirika wa kweli wa maendeleo ya jamii ya Watanzania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!