Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mabasi 100 Kupeleka Mashabiki Kwa Mkapa Kushangilia CHAN

  • 54
Scroll Down To Discover

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, ametangaza maandalizi ya mabasi takribani 100 kwa ajili ya kuwapeleka mashabiki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia na kushangilia mashindano ya CHAN.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Julai 30, jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha mashabiki wanapata fursa ya kuisapoti timu ya taifa katika mashindano hayo muhimu.

“Tumeshirikiana na wizara kuhakikisha mabasi ya kutosha yanapatikana. Wakuu wa wilaya wameshaelekezwa kuratibu usafiri huu kwa ufanisi, kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam hadi uwanjani na kurudi,” alisema Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila

Aidha, aliwahamasisha wafanyabiashara wadogo kuendelea na shughuli zao siku ya mashindano hayo, akisema kuwa fursa ya kiuchumi pia ipo wazi katika tukio hilo kubwa.

Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kuibua msisimko mkubwa jijini Dar es Salaam, huku mkoa huo ukiwa mstari wa mbele katika maandalizi ya kuhakikisha mashabiki wanashiriki kwa wingi.



Prev Post Zaidi ya asasi 167 kutoa elimu ya mpiga kura
Next Post Meridianbet Yawafikia Wasafishaji Wa Barabara Kinondoni, Yagawa Vifaa Vya Kujikinga Wakati Wa Usafi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook