
Ukiambiwa mapenzi ya kweli bado yapo, usibishe! Hili hapa ni mfano hai wa penzi la dhati na la kuponya roho.
Ni kati ya Mchungaji Leonard wa Kanisa la Pentekoste, Tukuyu mkoani Mbeya, na mrembo wake wa moyo, Eliza Sebastinia, ambao hivi karibuni wanatarajia kusimama madhabahuni na kufunga ndoa takatifu.
Timu ya Global TV imefunga safari hadi wilayani Tukuyu na kufanya mahojiano ya kipekee na wapenzi hao, ambapo walielezea kwa hisia na bashasha safari yao ya mapenzi – kutoka kwa mitazamo ya awali hadi sasa wanapojitayarisha kuanza maisha mapya kama mume na mke.
“Siku ya kwanza kabisa kumuona Eliza uso kwa uso… alinikaribisha kwa bashasha ya ajabu! Nilihisi amani na furaha ya ajabu ndani ya moyo wangu,” alisimulia Mchungaji Leonard kwa furaha.
Kwa upande wake Eliza, alieleza kuwa hakutazamia kuwa mtu wake wa maisha angekuwa mtumishi wa madhabahu, lakini alipogundua moyo wa upendo, uaminifu na maono aliyonayo Leonard, alijua penzi hili limetumwa na Mungu mwenyewe.
Wawili hao sasa wanahesabu siku chache kuelekea harusi yao, wakishirikiana na familia, ndugu, na waumini wa kanisa katika maandalizi ya siku hiyo ya kihistoria.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!