
KAMPUNI ya Usambara Research Training & Consultancy inayojishughulisha na masuala ya Utafiti Mafunzo na Ushauri wa Kitaalamu imevishauri Vyuo Vikuu vilivyopo nchini kufanya kazi na kampuni hiyo ili kupata utaalamu wa matumizi sahihi ya Akili Mnemba (AI) wakati wanatekeleza majukumu yao.
Pia imeziasa Taasisi za umma na binafsi kufanya kazi na kampuni hiyo ili kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benard Adam amesema Usambara imebaini wanafunzi wengi wa elimu ya juu hawana utaalamu wa kutosha juu ya kuandika tafiti kutokana na kukosa ujuzi.
” Kukosekana kwa ujuzi na utaalamu wa kuandaa tafiti kumewafanya wanafunzi wengi wa elimu ya juu kutumia kazi zilizofanywa na watu wengine wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kufanya tafiti,” amesema Adam.
Amesema Usanbara kwa kiliona hili wameamua kuanzisha kitengo maalumu cha kutoa mafumzo kuhusu namna bora ya kuandika tafiti kwa kutumia Akili Mnemba ( AI) sambamba na kuziandaa.
Ameongeza hatua hii itawawezesha wanafunzi kupunguza muda wa kuandika tafiti zao na kuzikamilisha kwa wakati.
“Suala la mafunzo halikuwaacha nyuma walimu hususan wa vyuo vikuu wanaosimamia tafiti hizo kwa kuwapatia mafunzo sahihi ya kubaini wanafunzi waliotumia AI kuandaa tafiti zao na namna bora ya kutumia AI,” amesema Adam
Kwa upande wa Taasisi za Umma , Binafsi na Wadau wengine amewataka kufanya kazi na kampuni hiyo ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzipatia suluhu kwa faida yao, jamii na taifa
“Usambara Research & Consultancy tunayasihi mashirika ya umma,binafsi na wadau wengine kututumia katika tafiti,mafunzo na ushauri wa kitaalamu ili kuleta suluhisho la matatizo mbalimbali katika maeneo yao kwa faida ya jamii na taifa,” amesema Adam.
Amefafanua kuwa mbali na shughuli hiyo pia kampuni inatoa msaada wa kurekebisha lugha kwenye tafiti sambamba na kupima Akili Mnemba AI pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.
Amesema mafunzo yanayotoewa na Kampuni ya Usambara huendeshwa na wahadhiri wabobevu kutoka Vyuo Vikuu vyenye Ithibati na kwamba ushauri wa kitaalamu hutolewa na walimu wa vyuo hivyo
vyenye ithibati na wahadhiri mahiri katika kutoa ushauri.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!