Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Akili Mnemba Yavumbua Dawa Mpya Zinazoweza Kupambana na Kisonono Sugu na MRSA

  • 7
Scroll Down To Discover

Watafiti wametangaza uvumbuzi wa aina mbili za dawa mpya za kupambana na maambukizi sugu (antibiotics) zinazoweza kuua vimelea vya kisonono sugu na MRSA.

Dawa hizo, zilizotengenezwa na Akili Mnemba kwa kutumia chembe ndogo sana, zimeonyesha uwezo wa kuua bakteria hao katika majaribio ya maabara yaliyohusisha wanyama.

Ingawa michanganyiko hii miwili bado inahitaji miaka ya uboreshaji na majaribio ya kimatibabu kabla ya kutumika kwa wagonjwa, timu ya Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) inasema uvumbuzi huu unaweza kuanza “enzi mpya ya dhahabu” katika ugunduzi wa dawa za kuua bakteria.

Hii ni hatua muhimu kwani maambukizi sugu sasa yanasababisha vifo vya zaidi ya milioni moja kila mwaka. Matumizi kupita kiasi ya dawa za bakteria yamesababisha bakteria kubadilika ili kuepuka athari za dawa, huku uhaba wa dawa mpya unaendelea kwa miongo kadhaa.



Prev Post Mpina Achukua Fomu ya Urais kwa Tiketi ya ACT-Wazalendo
Next Post Jeshi la Magereza latangaza nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook