

Akizungumza wakati wa sherehe ya kukata keki pamoja na wateja wao, ambayo imefanyika Temeke jijini Dar-es-Salaam Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania,Epimack Mbeteni amesema kuwa huduma zake zilianza Agosti 15, 2000, hivyo Kampuni hiyo inajivunia mafanikio makubwa ambayo yamerahisisha mafanikio makubwa kwa wateja wao ikiwa na mageuzi makubwa katika huduma za kifedha mpaka Sasa.

“Kama mnavyofahamu Vodacom Tanzania tunasherehekea miaka 25 ya M-Pesa tangu tumeanza na siku kama ya leo ya Agosti 15 ndio tulizaliwa ,hivyo tumekuja mtaani kuileta M-Pesa.Tunaita M-Pesa kitaani
“Tupo hapa kuzungumza na wateja wetu, na pia tutatoa zawadi kwa wateja wetu ambapo tupo nao kipindi chote mpaka Sasa, tutapita mtaani tutazungumza nao tusikia wanatuambia nini kuhusiana na Vodacom na M-Pesa .Pale tunapofanya vizuri na wapi wanataka tuboreshe na tutaboresha.

“Kwa hiyo ni siku ambayo tumeitoa kwa wafanyakazi wote wa Vodacom kuja sokoni kukaa na wateja, kuzungumza, kuwasikiliza ,kutatua changamoto zao, na kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo kusajiri line,hii ni Katika kufikia wateja wetu kwa wepesi zaidi na
pia kuwapa zawadi ambazo tutawapatia katika kusherehekea Birthday yetu Hivyo tutapita hadi Katika Soko la Temeke Stirio na kuwapa zawadi.
“Kama mnavyofahamu wakati M-Pesa inaanza watanzania waliokuwa wanaweza kupata huduma jumuishi za kifedha ilikuwa ni kama asilimia 9 kupitia benki lakini sasa hivi huduma za kifedha kwa Watanzania ni asilimia 76 ikichangiwa na huduma kama M- Pesa ambayo imeweza kuwafikia nchi nzima,

“Pia huduma nyingi ambazo zinatatua changamoto za kawaida za Watanzania leo hii tuna huduma ya M-Koba inayowasaidia akina mama katika vikundi vyao vya VICOBA kuweka fedha zao.Kuna huduma ya mikopo kama Songesha ambazo zimerahisisha huduma za mikopo nchi nzima kupitia simu yako unaweza kupata huduma,
“Tunahuduma nyingi ambazo tumezizindua katika miaka hii yote kubwa zaidi tumeleta mapinduzi kwa maana huduma zetu ambazo tumezianzisha nabaadae wengine wameziiga lakini tunajivuni tumewafikia watanzania kwa ukubwa zaidi.”
“Huko nyuma Watanzania wanafahamu huduma za kifedha zilikuwa zinapatikana kwa kupanga foleni kama foleni ya kuchota maji, kupata mkopo wa Sh.10,000 tu ilikuwa inabidi uombe ubebembeleze lakini sasa hivi kupitia simu yako unamaliza kila kitu kwa M-Pesa.

“Ukitaka kukata bima,kuwekeza, unataka fedha, mkopo ,kulipia bidhaa,kununua bandle na chochote unachokifanya unapata kupitia M -Pesa , kwahiyo kila kitu unakipata hivyo katika miaka 25 tumefanya mapinduzi makubwa katika huduma za kifedha nchini Tanzania.’ amesema,”Mbeteni.
Kuhusu usalama wa fedha za mteja amesema kuwa katika kipindi cha miaka 25 M-Pesa imekuwa salama sana na wateja wao wanasema moja ya sababu wanaamini usalama M-pesa kwani fedha zao ziko salama na hata ikitokea changamoto wanajua watahudumiwa na hizo ndizo sababu zinazotutofautisha Vodacom na wengine.
Nae Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania,Bi. Brigita Shirima amesema kuwa wafanyakazi wao wanazinguka Nchi nzima lengo ni kuwashukuru kwa kuwa nao na pia wanaendelea kuboresha huduma zao kwa kuongeza minara na kuongeza Ubora ili waweze kutoa huduma kila mahali Tanzania na kuendelea kuwafikia wateja wengi zaidi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!