

Dodoma, Agosti 15, 2025 – Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele, leo amekabidhi rasmi fomu za uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, Jijini Dodoma.
Mhe. Mpina aliambatana na mgombea wake wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, ambapo wote walithibitisha nia yao ya kushiriki katika uchaguzi wa mwaka huu chini ya tiketi ya ACT-Wazalendo.
Hii ni hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi, ikizingatia kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ndio chombo rasmi kinachosimamia taratibu za kisheria za kugombea nafasi za uongozi nchini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!