

Azania Bank imeshiriki kikamilifu katika maonesho ya Nanenane mwaka huu katika mikoa Saba ya Dodoma, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Simiyu, Tabora na Zanzibar. Maonesho hayo yalihitimishwa kitaifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.
Azania Bank imetumia maonesho hayo kutoa elimu ya masuala ya kifedha na namna ambavyo benki hiyo inaweza kuwakomboa wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi kupitia huduma zake mbalimbali chini ya kauli mbiu yake ya ‘Benkika Kidijitali Mpaka Shambani’ ambapo mkulima anaweza kupata huduma za kibenki hata akiwa shambani kwa kutumia simu yake ya mkononi. 





Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!