Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NMB YAENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA ZANZIBAR 

  • 33
Scroll Down To Discover

Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano na wateja wake visiwani Zanzibar kupitia mikutano ya ana kwa ana na wateja wakubwa, sambamba na kutoa elimu kuhusu masuluhisho mbalimbali inayoyatoa kwa wafanyabiashara.

Ujumbe wa benki hiyo, ukiongozwa na Meneja Biashara wa NMB Zanzibar, Bi. Naima Said Shaame, akiwa ameambatana na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara, Dickson Richard, pamoja na viongozi wengine wa benki, umekutana na wateja wakubwa katika ziara maalum ya kikazi.

Ziara hiyo inalenga kuendeleza ukaribu na kujenga uaminifu kati ya NMB na wateja wake, huku ikilenga kuhakikisha huduma na bidhaa zinazotolewa zinaendana na mahitaji halisi ya wateja.

Kwa miaka mitatu mfululizo, Benki ya NMB imetambuliwa kama Benki Salama Zaidi Tanzania (Safest Bank in Tanzania) na jarida la Global Banking & Finance Magazine, kuthibitisha ubora wake na kutambulika kimataifa katika nyanja mbalimbali za huduma za kifedha.

Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Shaame aliwashukuru wateja wote waliohudhuria na kuwasihi waendelee kuwa mabalozi wa Benki ya NMB kwa kuwaleta wateja wapya. Pia aliwaomba kuhakikisha kuwa mauzo na malipo yote ya biashara zao yanapitishwa kupitia akaunti zao za NMB ili kuongeza fursa ya kupata mikopo mikubwa zaidi kutoka benki yao.

Bi. Shaame aliongeza kuwa ubunifu unabaki kuwa nguzo kuu ya NMB, na benki itaendelea kuibua masuluhisho bora yatakayoongeza tija kwa wateja na kuchochea ukuaji wa biashara zao.



Prev Post Mkutano wa Maafisa Wakuu Jeshi la Polisi Moshi Kufunguliwa na Makamu wa Rais Dkt. Mpango
Next Post Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Mazishi Ya Hayati Ndugai
Related Posts
© Image Copyrights Title

TRA yawataka mawinga kulipa kodi

© Image Copyrights Title

TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook