Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Hayati Job Ndugai Aagwa kwa Heshima Kongwa, Azikwa Kijiji cha Madumbwa

  • 9
Scroll Down To Discover

Leo, Agosti 11, 2025, mamia ya waombolezaji wakiwemo waumini, viongozi wa serikali na vyama vya siasa wameungana katika Kanisa la Mtakatifu Michael Anglikana, Kongwa, kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Kongwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Hayati Job Ndugai.

Ibada ya mazishi iliongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana nchini, Dk. Maimbo Mndolwa, ambaye alitumia fursa hiyo kumwomba Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, kuendeleza miradi iliyokuwa imeanzishwa na marehemu, ikiwemo ujenzi wa hosteli katika kanisa hilo.

Baada ya ibada, mwili wa Hayati Ndugai ulisafirishwa hadi Kijiji cha Madumbwa, Kata ya Sejeli, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, ambako mazishi yalifanyika. Waombolezaji walimwaga machozi na kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo aliyehudumu kwa muda mrefu katika siasa na uongozi wa taifa.

Mazishi ya Ndugai yameacha kumbukumbu ya heshima na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Kongwa na Watanzania kwa ujumla, huku wengi wakikumbuka mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jimbo na taifa.



Prev Post Waziri Mkuu Amwakilisha Rais Dkt. Samia Mazishi Ya Hayati Ndugai
Next Post CRDB Yazindua Hatifungani ya Kwanza Isiyo na Riba kwa Wawekezaji wa Kiislamu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook