Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mkutano wa Maafisa Wakuu Jeshi la Polisi Moshi Kufunguliwa na Makamu wa Rais Dkt. Mpango

  • 37
Scroll Down To Discover

Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Jeshi la Polisi nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi kuanzia Agosti 11 hadi 15, 2025 katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi pamoja na kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha na kudumisha usalama nchini ikiwemo ya kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika katika mazingira yenye amani, utulivu na usalama.

Mkutano huo, unatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 11, 2025.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime amesema Katika Mkutano huo pamoja na kufanya tathmini, mada mbalimbali zitawasilishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 11, 2025
Next Post NMB YAENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA ZANZIBAR 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook