Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Mkuu Majaliwa Atuma Salamu za Pole Kufuatia Kifo cha Job Ndugai

  • 43
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Majaliwa ameandika:

“Ninaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa salamu za pole kufuatia msiba wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Yustino Ndugai.

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape utulivu Familia, Wana Kongwa, Familia yote ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wana CCM wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.”



Prev Post Wasifu Wa Job Ndugai: Kuzaliwa, Elimu, Kujiingiza Kwenye Siasa Hadi Kifo – Video
Next Post Bei ya Mafuta Yapungua Dar, Yapanda Mtwara – EWURA Yatangaza Bei Mpya za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook