Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi, Ahudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri Jijini Dar

  • 42
Scroll Down To Discover

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 22 Juni, 2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali walivyowasili Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Juni 22, 2025.

Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Serikali wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa, kupanga mikakati ya maendeleo na kutathmini utekelezaji wa sera mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri.
Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa Kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 22 Juni, 2025.



Prev Post Waziri Dkt Stagomena Awatunuku Shahada ya Uzamili na Stashahada Maafisa 71
Next Post Jeshi la Polisi Lafafanua Ukamatwaji wa Wachokonozi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook