Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Dkt Stagomena Awatunuku Shahada ya Uzamili na Stashahada Maafisa 71

  • 37
Scroll Down To Discover

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt Stagomena Tax ametunuku Shahada ya uzamili na Stashahada kwa Maafisa 71 kutoka nchi 14 za Afrika katika Mahafari ya 39 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania leo tarehe 21 Juni 2025.
Akizungumza wakati wa Mahafari hayo, Dkt Tax amewaasa wahitimu wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutumia ujuzi walioupata kutoka chuoni hapo kushiriki katika uandaaji na upangaji wa mikakati ya kiusalama wa mataifa yao ili kulifanya Bara la Afrika mahala salama.
Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali  Stephen Justice Mnkande amesema kuwa Maafisa hao wamehitimu na kutunukiwa shahada ya Uzamili na Stashahada ya Juu Defence and Security Studies ambapo wamefaulu kwa viwango vya juu.
 Naye Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Salum Haji Othman amesema kuwa Maafisa hao wanategemewa na Majeshi ya mataifa yao katika kusaidia kupanga mikakati mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa mataifa yao na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa katika utatuzi wa changamoto za kiusalama katika nchi zao.
Maafisa waliohitimu katika Mahafari hayo ni kutoka nchini Tanzania, Burundi, DRC, Eswatini, Ethiopia, Kenya, Malawi, Misri, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Uganda na Zambia.



Prev Post Rais Samia Aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Dar – Picha
Next Post Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi, Ahudhuria Kikao cha Baraza la Mawaziri Jijini Dar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook