
Jeshi la Nepal litaanza tena mazungumzo na waandamanaji wa “Gen Z” siku ya leo Alhamisi ili kuamua kiongozi mpya wa muda wa taifa hilo la Himalaya, msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema baada ya maandamano ya hasira na kuua 30 na kulazimisha waziri mkuu kujiuzulu.
Wanajeshi walishika doria katika mitaa tulivu ya Kathmandu, mji mkuu, baada ya kushuhudiwa kwa maandamano mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miaka kadhaa nchini humo yaliyochochewa na marufuku ya mitandao ya kijamii ambayo mamlaka iliirejesha tena baada ya vifo 19 huku polisi wakifyatua mabomu ya machozi na risasi za mpira kuudhibiti umati wa watu.
“Mazungumzo ya awali yanaendelea na yataendelea leo,” Raja Ram Basnet, ameiambia Reuters, yakiwa ni majadiliano ya kumpata kiongozi mpya wa muda. “Tunajaribu kurekebisha hali polepole.”
Wizara ya afya ya Nepal imesema idadi ya waliofariki kutokana na maandamano hayo imeongezeka hadi 30 kufikia leo Alhamisi, huku 1,033 wakijeruhiwa.
Maagizo ya marufuku ya kutotoka njeiliyowekwa katika mji mkuu wa Kathmandu na maeneo ya karibu kwa siku nzima itaendelea kwa mujibu wa taarifa ya jeshi huku msemaji wa uwanja wa ndege akibainisha kuwa safari za ndege za kimataifa zimeendelea kama kawaida.
Maandamano hayo yanajulikana kama maandamano ya “Gen Z” kwa kuwa washiriki wengi walikuwa vijana wakielezea kusikitishwa na kushindwa kwa serikali kupambana na rushwa na kukuza fursa za kiuchumi.
Waandamanaji wamemtaka Jaji Mkuu wa zamani Sushila Karki kama waziri mkuu wa muda, kwa mujibu wa Raman Kumar Karna, katibu wa Chama cha Wanasheria wa Mahakama ya Juu, ambaye walishauriana naye.
Maandamano hayo yameshuhudia majengo ya serikali, kuanzia mahakama kuu hadi nyumba za mawaziri, ikiwa ni pamoja na makazi ya kibinafsi ya Oli, yakichomwa moto, na kupungua baada ya waziri mkuu kujiuzulu. Pia hoteli kadhaa katika mji wa kitalii wa Pokhara na Hilton huko Kathmandu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!