Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA MPYA HII HAPA….MO DEWJI AJIWEKA KANDO…TRY AGAIN APIGWA CHINI…MAGORI, BARBARA WAULA…

  • 39
Scroll Down To Discover

Simba imefanya mabadiliko makubwa ya Bodi ya Wakurugenzi baada ya mwekezaji Mohammed Dewji ‘MO’ akijiweka kando, huku akimteua Crescentius Magori kuchukua nafasi hiyo, ilihali CEO wa zamani wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez akirejea klabuni.

Mabadiliko hayo ambayo yametangazwa dakika chache zilizopita, MO mbali na Magori aliyewahi kuwa, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo na mshauri wa Mo Dewji ameteua sura mpya nne, huku watatu wakitoka Bodi iliyopita.

Wajumbe wapya wanne katika Bodi hiyo ni pamoja na mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani, Swedy Mkwabi, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na George Ruhango.

Barbara alitangaza kujiuzulu Simba Desemba, 2022 japo nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu aliiacha rasmi Januari 10, 2023 akiwa mmoja ya viongozi walioweka heshima klabuni hapo, hasa kwa mafanikio ya Simba kimataifa.

Wengine ni Zuly Chandoo, wakati Rashid Shangazi na Hussein Kitta wakiendelea kwenye Bodi hiyo.

Kwenye Uteuzi huo jina kubwa lililoshtua likikosekana ni Salim Mhene ‘Try Again’ aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Taarifa hiyo haijaweka wazi sababu za kuondolewa kwa Try Again ambaye alikuwa Mjumbe aliyedumu kwa muda mrefu kabla ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

The post SIMBA MPYA HII HAPA….MO DEWJI AJIWEKA KANDO…TRY AGAIN APIGWA CHINI…MAGORI, BARBARA WAULA… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Israel yapuuza pendekezo la Hamas ili kumaliza vita. Katika Dira ya Dunia TV
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 05, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook