
Wananchi wa Boma Ng’ombe, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika tarehe 01 Oktoba, 2025.
Mkutano huo ulivuta hisia kubwa za wananchi waliokusanyika kusikiliza sera na mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi. Shamra shamra, nyimbo na nderemo vilitawala uwanjani huku wafuasi wa CCM wakionesha mshikamano na kuunga mkono wagombea wao.
Viongozi wa chama hicho walitumia nafasi hiyo kueleza mafanikio yaliyopatikana na kuahidi kuendelea kusimamia maendeleo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii, miundombinu na uchumi wa wananchi wa Hai na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!