Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kikwete Awaasa Watanzania Kudumisha Umoja Na Amani – Video

  • 2
Scroll Down To Discover

KIBAHA, PWANI – Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia wananchi wa Kibaha katika kampeni, amesisitiza kuwa Tanzania inabaki kuwa mfano wa amani na mshikamano barani Afrika licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120, watu wa rangi tofauti na waumini wa dini mbalimbali.

“Nchi yetu ina umoja. Nchi yenye makabila 120 wa rangi mbalimbali, waumini wa dini mbalimbali, lakini hakuna ugomvi wa kikabila, hakuna ugomvi wa kidini, wala hakuna ugomvi wa maeneo,” alisema Kikwete huku akipongezwa kwa makofi na shangwe kutoka kwa wananchi.

Dkt. Kikwete ameongeza kuwa mshikamano huo ni nguzo muhimu katika kulinda amani, mshikikiano na maendeleo ya taifa.

Alisisitiza pia kumwezesha kwa kumpatia wabunge na madiwani wa CCM ili aendelee kutekeleza majukumu yake bila vikwazo.

Kikwete alimpongeza Dkt. Samia kwa kuendelea na kampeni akiwa na afya njema na nguvu licha ya ziara katika mikoa mbalimbali.



Prev Post Dkt. Samia Aahidi Ujenzi wa Bandari Mpya ya Bagamoyo – Video
Next Post Zari The Bosslady Apata Ajali ya Gari, Range Rover Yake Yaharibika
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook