Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mtoto wa Ndugai Ampongeza Rais Samia, Atoa Shukrani Kwa Niaba ya Familia – Video

  • 12
Scroll Down To Discover

Mtoto wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Ndugai, Yustino Ndugai.

Mtoto wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Ndugai, Yustino Ndugai, ametoa salamu za shukrani kwa niaba ya familia mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mamia ya waombolezaji waliokusanyika kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli ya kumuaga.

Katika hotuba yake, Yustino alieleza kuwa familia inatoa shukrani za dhati kwa Rais Samia, Serikali, Bunge, viongozi wa dini, wananchi na wote walioshiriki katika kipindi chote cha msiba, akisema upendo na mshikamano uliodhihirishwa umeifariji familia katika wakati huu mgumu.

Shughuli ya kumuaga Hayati Ndugai imefanyika leo mjini Dodoma, kabla ya mwili wake kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Kongwa kwa mazishi yatakayofanyika kesho.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 10, 2025
Next Post Rais Samia: Hayati Ndugai Alikuwa Mkomavu Kisiasa Na Kiuongozi (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook