Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia: Hayati Ndugai Alikuwa Mkomavu Kisiasa Na Kiuongozi (Picha +Video)

  • 33
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waombolezaji kabla ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 10 Agosti, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Hayati Job Yustino Ndugai alikuwa kiongozi mkomavu kisiasa na kiuongozi, ambaye aliweka thamani kubwa katika demokrasia ya Bunge.

“Hayati Ndugai alikuwa mkomavu kisiasa na kiuongozi, na aliyeamini katika demokrasia ya Bunge. Alipokuwa Spika, Bunge lilishuhudia mafanikio mbalimbali yaliyoelezwa hapa na Katibu wa Bunge lakini pia Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Rais Samia.

Rais Samia aliyasema hayo tarehe 10 Agosti 2025, katika viunga vya Bunge jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ndugai, aliyefariki dunia hivi karibuni. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wabunge, ndugu, jamaa na wananchi waliojitokeza kumuenzi marehemu.

Rais Samia akiwafariji wanafamilia wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 10 Agosti, 2025.



Prev Post Mtoto wa Ndugai Ampongeza Rais Samia, Atoa Shukrani Kwa Niaba ya Familia – Video
Next Post Rais Samia Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Hayati Job Ndugai (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook