Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia: Tukomeshe Makundi Baada Ya Uteuzi, Tujikite Katika Umoja Wa CCM – Video

  • 44
Scroll Down To Discover


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kote nchini kuweka kando makundi na tofauti za mitazamo mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia amesema mshikamano na umoja ndani ya chama ni silaha muhimu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

“Mchakato wa uteuzi unapoisha, na makundi pia nayo yaishe, na ushindani ndani ya chama pia uishe. Tunarudi kuwa kitu kimoja ili tuingie kwenye uchaguzi mkuu, CCM ikiwa chama madhubuti, chama kimoja chenye umoja na mshikamano,” amesema Dkt. Samia.

 



Prev Post TRA Yasisitiza Mawinga Wachangie Maendeleo Kupitia Kodi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook