Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Suluhu Achukua Fomu za Kugombea Urais 2025 (Picha +Video)

  • 16
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa begi lenye nyaraka za Fomu ya uteuzi Ugombea Urais na Makamu wa Rais katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mkoani Dodoma leo August 09,2025

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 9, 2025, amechukua rasmi fomu za kugombea nafasi hiyo kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Shughuli hiyo imefanyika katika ofisi za makao makuu ya tume, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, ndiye aliyemkabidhi Dkt. Samia fomu hizo.

Dkt. Samia aliwasili katika ofisi za tume saa 5:20 asubuhi akiwa ameongozana na mgombea mwenza wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi, na viongozi wakuu wa chama akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuber Ali Maulid, pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

Baada ya kukamilisha taratibu za ndani kwa takribani dakika 27, Dkt. Samia alitoka akiwa amebeba begi jeusi lenye maandishi “Fomu za Uteuzi”, ishara ya kukamilika kwa hatua hiyo muhimu katika safari yake ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Nje ya jengo la INEC, mgombea huyo wa CCM alisimama kupiga picha na makundi mbalimbali ya makada na wafuasi wa chama, huku wakiwa na furaha na shangwe kubwa.

Mara baada ya hapo, msafara wa Dkt. Samia na mgombea mwenza wake ulielekea makao makuu ya CCM jijini Dodoma kwa ajili ya kuendelea na ratiba za chama, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kampeni rasmi.

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025.



Prev Post OCP Yaonesha Ubora wa Mbolea ya TSP Katika Maonesho ya Nane Nane Mbeya
Next Post TRA yawataka mawinga kulipa kodi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook