Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wa kati, maarufu Mawinga, kujitokeza kulipa kodi kama sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa.
Ameyasema hayo, Kamishna wa TRA, Yusuph Mwenda wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wawakilishi wa TCRA, BASATA na Umoja wa Wafanyabiashara wa Kariakoo katika uzinduzi wa Kampeni ya Elimu ya Kodi kwa Biashara za Mtandaoni uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Hatutakutoza kwa chote kile, kama wewe winga umechukua kitu kwa milioni 1 ukauza kwa milioni 1 na laki 1, huwezi kutozwa kwa milioni moja na laki 1 utatozwa kwa laki 1 ila utatusaidia huyo wa milioni 1 ni nani na yeye tukamtoze kodi,” amesema.
Kamishna Mwenda amefafanua kuwa ikiwa mawinga watalipa kodi kama inavyoelekezwa itazalisha faida nyingi zikiwemo kutambulika, kukopesheka na kutoonewa.
The post TRA yawataka mawinga kulipa kodi appeared first on SwahiliTimes.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!