Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto: Wanaongoja kusikia CCM imepasuka watasubiri kwa miaka mingi

  • 41
Scroll Down To Discover

Katibu wa Kamati Maalum vya NEC Zanzibar idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis

Na Mwandishi Wetu , Dodoma

Chama Cha Mapinduzi kimesema makundi ya Waganga njaa , Wanafiki na mamluki wanaosubiri kusikia CCM kimesambaratika watasubiri kwa miaka mingi ijayo na kamwe chama hicho hakitagawanyika .

Vile vile kimesisitiza mizizi ya CCM imefika mbali ardhini hivyo kukatika na kupoteza nguvu zake za asili ni kazi ngumu isiowezekana .

Katibu wa Kamati Maalum vya NEC Zanzibar idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ,amewataka wasaliti wote wazidi kukesha katika mitandao ya kijamii huku wakijua hawatabadili lolote .

Mbeto kwa upande mwingine , alimpongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza mkutano Mkuu wa Taifa kwa njia ya mtandao uliofanya marakebisho ya msingi ya katiba ya CCM.

Alisema kupitia mkutano Mkuu huo wa Taifa, kumefanyika Marekebisho muhimu ya Katiba yake hivyo sasa Kamati Kuu itakuwa na uwezo wa kupeleka majina ya wagombea zaidi ya matatu katika kikao cha NEC.

“Chama kwa dhati kabisa kinampongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia kwa kuonyesha umakini wa kuongoza mkutano Mkuu kwa mtindo wa aina yake . Kila kitu kimekwenda kwa murua kama ilivyokusudiwa” Alisema Mbeto.

Katibu huyo Mwenezi alisema awali kabla ya Marekebisho mapya , Kamati kuu ya CCM ilikuwa na mamlaka ya kupeleka majina matatu ya wagombea mbele ya NEC ambapo sasa inaweza kupeleka majina zaidi ya kumi.

“Chama chetu kila siku kinapata ustawi na kuungwa mkono na wawanachi. Nafasi moja inaweza kuwaniwa na Wanachama kati 40 hadi 50. Chama baada ya kutafakari, kimeona kupeleka majina matatu pekee si mantiki ya demokrasia ” Alisema

Aidha ,Mbeto alisema kwa bahati nzuri sasa majina ya wagombea yatapelekwa Nec kwa kadri Kamati itakavyoona inafaa kulingana na uhalisia na ushindani na idadi ya wagombea.

Pia Mwenezi huyo alisema kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na maneno mengi ikiwemo uvumi kuwa ndani ya CCM kuna mvutano, mgawanyiko na mpaasuko jambo ambalo alisema ni upuuzi mtupu.

“Waelezeni mamluki na wanafiki CCM ni chama kikongwe chenye Wanasiasa shupavu na viongozi wabobezi . Hakiongozwi kwa mihemko ya watu au kwa mitandao ya kijamii imeandika nini ” Alisisitiza Mwenezi huyo



Prev Post Bingwa wa Ballon D’OR na Meridianbet Huyu Hapa
Next Post ACT Wapokea Nakala Tepe Daftari La Wapiga Kura
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook