
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Julai 29, 2025, kimetangaza majina ya wagombea sita waliopitishwa kuwania ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia kura za maoni. Miongoni mwa walioteuliwa ni:
Ponela Matei
Habib Mchange
Allan Sanga
Henjelewe
Ally Mandai
Francis Elias
Kilichoibua mshangao zaidi ni jina la Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, kutokurudi kabisa kwenye orodha ya waliopitishwa, licha ya jina lake kuwahi kutajwa na kupewa nafasi kubwa.
Tangazo hilo limetolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, katika mkutano rasmi na waandishi wa habari uliofanyika leo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!