Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Namibia yamuapisha Rais wake wa kwanza mwanamke

  • 67
Scroll Down To Discover

Rais mpya wa Namibia ameapishwa leo siku ya Ijumaa kuongoza nchi inayokabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira, ukosefu wa usawa na umaskini.
Na atakuwa akikabiliana na changamoto za kiuchumi sambamba na kuwa Rais mwanamke wa pili kuwahi kuchaguliwa moja kwa moja barani Afrika na Rais wa kwanza mwanamke wa Namibia.
"Ikiwa mambo yataenda vizuri basi itaonekana kama mfano mzuri," Netumbo Nandi-Ndaitwah aliambia podikasti ya BBC Africa Daily.

"Lakini kama jambo lolote likitokea, kama linaweza kutokea katika utawala wowote chini ya wanaume, kuna wale ambao wangependa kusema: 'Waangalie wanawake!'

Akiwa na umri wa miaka 72 alishinda uchaguzi kwa 57% ya kura huku mpinzani wake wa karibu Panduleni Itula akipata 26% ya kura, kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Ni kisa katika mfululizo wa matukio katika maisha yake- Nandi-Ndaitwah akipigana na utawala uliokuwa, na kutoroka kisha kujiwezesha na kujijenga kama mwanamke mashuhuri nchini Namibia.
Nandi-Ndaitwah amekuwa mwanachama mwaminifu chama tawala cha SWAPO tangu akiwa msichana na kuapa kuleta mabadiliko ya kiuchumi Namibia.
Nandi-Ndaitwa alizaliwa 1952 ,kaskazini mwa kijiji cha Onamutai.
Ni mtoto wa tisa miongoni mwa watoto 13 na babake mzazi alikuwa kiongozi wa kidini wa kanisa la Anglikana.
Namibia ni nchi kubwa kijiografia yenye idadi ndogo ya watu milioni tatu.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa wakulima wa asili ya kizungu wanamiliki takriban asilimia 70 ya mashamba ya nchi hiyo
Jumla ya Wanamibia 53,773 waliotambuliwa kuwa wazungu katika sensa ya 2023, wakiwakilisha asilimia 1.8% ya wakazi wa nchi hiyo.
Kiwango cha ukosefu wa ajira kiliongezeka hadi asilimia 36.9% mnamo 2023 kutoka asilimia 33.4% mnamo 2018, kulingana na wakala wa takwimu nchini.
Nandi-Ndaitwah alisema uchumi ambao kwa kiasi fulani unategemea mauzo ya madini nje ya nchi unapaswa kufanya kazi zaidi katika kuongeza thamani ya kile ambacho nchi inachimba kutoka ardhini badala ya kusafirisha malighafi nje ya nchi.
Pia anataka Namibia kuangazia zaidi sekta za ubunifu na kufanya sekta ya elimu kuzoea hali halisi mpya ya kiuchumi.
Nandi-Ndaitwah ni mwanamke wa pili Mwafrika kuchaguliwa moja kwa moja kama rais, baada ya Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.
Rais mwingine mwanamke pekee wa bara hilo kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake kufariki dunia akiwa madarakani mwaka 2021.
Nandi-Ndaitwah anataka kupimwa kwa ubora wake, lakini alisema kuwa ni
"jambo zuri kwamba sisi kama nchi tunatambua kwamba kama vile wanaume [wanaweza kufanya], wanawake wanaweza pia kushikilia nafasi ya mamlaka".



Prev Post Putin atavunja makubaliano ya amani na Ukraine yasipolindwa - Uingereza
Next Post Marais 5 Waliouawa Kikatili Wakiwa Bado Madarakani....
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook